Social Icons

Featured Posts

Friday, September 30, 2016

RC Makalla afungua maonesho ya wajasiriamali kwa niaba ya Waziri wa Viwanda

 Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, ndugu Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya, akikagua bidhaa za Wajasiriamali wa kanda ya Nyanda za juu kusini leo, katika maonesho ya wajasiriamali lililoandaliwa na Shirika la viwanda vidogo (SIDO), ambapo maonesho hayo yanaendelea katika viwanja vya bustani ya Jiji la Mbeya mkabala na uwanja wa Sokoine.
 Mjasiriamali wa bidhaa za usindikaji kutoka wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, Sarah Kalinga akiwa katika banda lake katika viwanja vya Bustani ya Jiji la Mbeya leo wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo uliofanywa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Gabriel Makalla kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage.
 Bidhaa za wajasiriamali zikiwa kwenye mabanda yao.
 Mwamko mdogo na kuchelewesha kuanza kuyatangaza matangazo ya maonesho hayo, yamepelekea wananchi kutojitokeza vya kutosha katika maonesho hayo. Hapo SIDO wanapaswa kuwajibika.Thursday, September 29, 2016

MBEYA; Anselima grower four, mwandishi wa habari aliyetua kalamu na kuwa mjasiliamali

Anselima Komba (26),  ambaye kwa sasa ni mjasiliamali na sasa yupo katika viwanja vya maonyesho ya wajasiliamali wa kanda ya Nyanda za juu kusini viwanja vya Garden Jijini Mbeya.

Anasema ustaa bila uchumi ni bure.

Dawa za kulevya aina ya Mirungi na madhara yake

Na Gordon Kalulunga - Tanzania

MIRUNGI ni aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unevunyevu na milima yenye urefu wa kati ya futi 4000 hadi 9000.

Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika mikoa ya Arusha, Kilimajaro, Manyara na Tanga.

Hata hivyo kiasi kikubwa cha mirungi itumikayo nchini huingizwa isivyo halali kutoka nchini Kenya.

Mirungu hujulikana kwa majina mengi kama vile Miraa, Mbaga, Mogoka, Veve, Bomba na Kashamba.

Kwa mujibu wa wakala wa Maabara ya mkemia Mkuu wa Seriali ya Tanzania, Mirungi ina kemikali inayojulikana kama “Cathinone”, ambayo mtumiaji akitumia hukosa hamu ya kula.

Madhara mengine kwa mtumiji wa Mirungi ni kutokwa na vidonda vya mdomoni na tumboni, kukosa choo, kupungukiwa maji mwilini, kupata shinikizo la damu, kupungukiwa nguvu za kiume, mwili kuwasha, kupata maumivu makali ya kichwa na kuharibika ini.

Sheria ya dawa za kulevya ya mwaka 1995, inasema kuwa, ni kosa la jinai, kutumia, kuhamasisha matumizi, kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yeyote ile na mirungi.

Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha.

TAARIFA YA UPATIKANAJI WA DAWA


Vijana watakiwa kufanya kazi kwa bidii kuondoakana na umasikini


Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa kupata maendeleo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini ambao umekithiri nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akizungumza na vijana kuhusu ujasiriamali.
Alisema ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni muhusika mwenyewe kujiongeza kwa kufanya kazi kwa bidii katika jambo ambalo anatamani kulifikia na akiwatolea mfano yeye mwenyewe kuwa tangu amalize masomo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hajawahi kurudi chuoni kuchukua cheti chake lakini amefanikiwa kimaisha.
"Mimi simchukii mtu ila nauchukia umaskini alionao, ukiwa na juhudi katika biashara na kujituma hata Rais Magufuli hatakufikia mshahara watu wanaweza kusema unafanya biashara ya kawaida lakini inakulipa sana, ni wewe tu na juhudi zako unazofanya ili ufanikiwe,
"Maisha hayana formula kuwa kufanikiwa ni lazima uwe na masters ndiyo upate mafanikio, masters ya maisha ni kuwa mtaani maisha yakupige alafu uinuke upambane na uyashinde hapo ndiyo umeyashinda maisha, ukitaka kufanikiwa lazima ufanye kazi kwa bidii hata mimi natumia muda wangu mwingi kujifunza ili nizidi kufanikiwa," alisema Mashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kufanikiwa kimaisha kwa kufanya biashara.

Aidha Mashauri aliwataka vijana hao kutumia fursa ambayo inatolewa na kampuni yake ya kuuza vifaa vya viwandani ya HiTech International kwa kuwapatia mkopo wa mashine watu ambao wanatamani kufanya biashara za aina mbalimbali ili waweze kufanikiwa kama matajiri wengine wakubwa nchini wamevyofanikiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akiwaonyesha moja ya mashine ambazo Kampuni ya HiTech International inaziuza.
Nae mwendesha mafunzo kwa vijana hao kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Benny Mwambela alisema mafunzo hayo yameanzishwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ili kuwasaidia vijana kupata mbinu za jinsi gani wanaweza kufanikiwa kibiashara na baada ya mafunzo hayo, wahitimu watakwenda kutoa elimu kwa vijana wengine.
"Tunafundisha walimu ambao watakwenda kufundisha watu wengine kuhusu ujasiriamali, kuna watu wasiopungua 10,000 wamejiandikisha kujifunza ujasiriamali kwahiyo tunawafundisha watu hawa ili wakawafunze na wengine ili na wao wajue jinsi gani wanaweza kufanya biashara,
"Wanafundishwa jinsi ya kubuni wazo la biashara, kuna wengine wana mawazo ya biashara watafundishwa jinsi ya kuanzisha biashara, na kuna wengine wanafanya biashara wanafundishwa jinsi ya kutanua biashara na watafundishwa kuhusu kuanzisha vikundi na jinsi gani ya kutumia fedha," alisema Mwambela.

Wednesday, September 28, 2016

TAMWA YATAKA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KUTOA FURSA YA WANAWAKE KUSIKIKA.

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu, wakiwa kwenye semina iliyofanyika Jumamosi wiki iliyopita Septemba 23, 2016 Jijini Dar es salaam. 

Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, ambapo pamoja na mambo mengine iliangazia kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari kuhusu mafanikio na changamo za wanawake ili kufanya jamii iwatambue na hivyo kuwafunguliwa fursa mpya ikiwemo kujitokeza kwenye masuala ya uongozi.
Na BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok  Mayombo, akifungua semina hiyo.
Kushoto ni mkufunzi katika semina hiyo, Valerie Msoka ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya InterNews tawi la Tanzania. Pia ni Mkurugenzi mstaafu wa TAMWA.
Godfrida Jola ambaye ni Afisa Miradi TAMWA, akizungumza jambo kwenye semina hiyo
Mshiriki
Mshiriki kutoka Kanda ya Ziwa
Mshiriki
Mmoja wa wanasemina
Wanasemina
Mmoja wa wanasemina akichangia jambo
Wanasemina kwenye majadiliano
Wanasemina kwenye majadiliano
Wanasemina kwenye majadiliano
Makabidhiano ya nakala mbalimbali kutoka TAMWA
Kulia ni Godfrida Jola kutoka TAMWA na kushoto ni George Binagi-GB Pazzo kutoka Lake Fm Mwanza & BMG.
*****************************************
Vyombo vya habari nchini vimehimizwa kutoa fursa kwa wanawake kuonesha umahiri wa utendaji wao wa kazi ili kuleta chachu kwa wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA, Alakok  Mayombo, alitoa rai hiyo jumamosi iliyopita kwenye mafunzo kwa wanaandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu yaliyofanyika jijini dar es salaam.

Alisema bado idadi ya wanawake walio kwenye nafasi mbalimbali za uongozi serikalini ni chini ya asilimia 30 kwa nchi za kusini mwa Bara la Afrika ikiwemo Tanzania hivyo waandishi wa habari wana nafasi kubwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yaliandaliwa na TAMWA, walisema mafunzo hayo yawatawasaidia kuandaa vipindi bora vitakavyowahamasisha wanawake nchini kujitokea kuwania nafasi za uongozi katika jamii.
                           Soma HAPA Mafunzo ya Kanda ya Ziwa

Dawa za kulevya aina ya Cocaine


Na Gordon Kalulunga-Tanzania

Makundi rika na kuiga ni moja ya sababu inayopelekea baadhi ya vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo Bangi, Mirungi, Cocaine, Petrol na vileo mbalimbali.

Leo naangazia dawa za kulevya aina ya Cocaine ambayo inatengenezwa na mmea uitwao Coca ambao unastawishwa katika nchi za America ya kusini.

Dawa hii ipo katika kundi la kichangamshi kikali ambacho huathiri mfumo wa fahamu.

Cocaine huwa katika unga mweupe au katika hali ya mawe madogo madogo.

Majina ya mtaani huitwa unga. White suger, keki, big c, bazooka, snow na unga mweupe.

Kinachotokea baada ya kutumia Cocaine, mtumiaji huchangamka kupita kiasi, kupungua kwa mboni za macho, kupungua kwa hamu ya kula, kukauka koo, kutokutulia, kuwa na mhemko wa kufanya ngono, kusinyaa kwa mishipa ya damu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

Madhara kwa mtumiaji ni kuwa na maono au njozi zisizo za kweli, kuchanganyikiwa, kuwashwa mwilini, kuwa na hasira za ghafla, hisia za uwepo wa vijidudu mwilini, kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo kunakoweza kusababisha kiharusi au kifo, kuongezeka na kupungua kea mapigo ya Moyo ghafla, kutetemeka kwa nguvu kama kifafa, utegemezi, kuvunja Sheria na matatizo ya kisaikolojia.

Uwepo wa mwathirika mmoja, jamii nzima inaathirika.

Kutumia dawa za kulevya kunachochea zaidi kupata magonjwa yatokanayo na ngono ukiwemo Ukimwi.

Tuungane kutoa elimu na kupinga matumizi ya dawa za kulevya nchini ili jamii yetu iwe salama.

Tuesday, September 27, 2016

SAUTI KUTOKA NYIKANI; Dawa za kulevya na madhara yake

Na Gordon Kalulunga, Mbeya.

Leo tuangazie dawa za kulevya aina ya Heroin ambayo inatokana na mmea unaojulikana kama Afyuni (Opium poppy).

Kilimo cha mmea huo hufanyika kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Afghanistan. Pia mmea huo unalimwa kidogo katika nchi ya Misri.

Dawa hii ya kulevya ipo katika kundi la Vipumbaza ambapo hupumbaza mfumo wa fahamu na kumsababisha mtu kusinzia, kupungua kwa mawazo na maumivu ya mwili.

Heroin huingizwa hapa nchini Tanzania kwa njia mbalimbali kama vile anga na maji ikitokea nchi za mashariki ya mbali.

Majina mengine ya Heroin ni unga, brown sugar, ngoma, ubuyu, mondo, Duke, farasi na Ponda.

Madhara yake kwa watumiaji ni kuharibika kwa mfumo wa fahamu, kupata njozi, mabadiliko ya hedhi kwa wanawake na hujenga hali ya uteja kwa haraka kuliko dawa nyingine ya kulevya.

Kwa wanaojidunga huweza kuambukizana Virusi vya Ukimwi, dozi kubwa husababisha vifo.

Ikichanganyika na pombe madhara yake ni makubwa zaidi pamoja na kifo, kizunguzungu, kichefuchefu na kufunga choo.

Kutotumia na kuacha dawa za kulevya inawezekana.

Tanzania Yetu. Mitindo Yetu.


MBEYA; Mbunge Oran Njeza aongoza mazishi ya kada wa CCM

 Mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Oran Njeza, akiongoza waombolezaji wa msibani wa kada wa CCM mjini Mbalizi Neema Mroso aliyefariki jana baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha Kali na mtu/watu wasiojulikana.

(Picha na Solomon Mwaisengela).
 Mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini Oran Manase Njeza, (kushoto), akiwa na aliyekuwa mgombea nafasi ya udiwani kata ya Utengule Usongwe jimboni humo ndugu Ntunjilwa katika eneo la maziko mjini Mbalizi walipokwenda kumhifadhi aliyekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo Neema Mroso. 

(Picha na Matatizo Kameka).
Kushoto ni Marehemu Neema Mroso enzi za uhai wake.